MKUU wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile amewataka wanaume kuwapeleka wake zao kuhudhulia kliniki wanapokuwa wajawazito pamoja na kuhakikisha wanakula vizuri.
Hayo ameyasema katika Kikao cha tathimini ya utekelezaji wa afua za Lishe kwa kipindi cha robo ya tatu Januari hadi Machi 2023.
Ndile amesema akinamama wajawazito wamekuwa na mwitikio mdogo kwaajili ya Semina juu ya Lishe hivyo kusababisha kati ya watoto 10 wanaozaliwa 3 kuzaliwa na uzito mdogo.
Mkuu wa Wilya amesema wamama wajawazito wapewe Elimu ya Lishe bora ili watoto wazaliwe na uzito mzuri ikiwa akina baba kufuatilia Afya zao kwa ukaribu.
Hata hivyo Ndile amemwagiza Afisa Elimu Msingi kuwaandikia walimu wa Shule za Msingi kuhakikisha wanasimia watoto wote kula shuleni.
“Nasisitiza Mimi Mkuu wa Wilaya,Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Halmashauri popote tutakapopita tutahimiza habari za uchangiaji wa chakula mashuleni”.
Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Mussa Rashid akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed amesema mara nyingi kinachopelekea watoto kuzaliwa na uzito mdogo akina mama wajawazito kuchagua aina ya vyakula.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Habari Halamshauri ya Wilaya ya Madaba
Mei 9,2023
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa