MWENYEKITI wa Kijiji cha Lituta Halmashauri ya Madaba Beno Mwenda ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha shilingi Milioni 190 kwaajili ya ujenzi wa Soko la Kihistoria.
Mwenda amesema katika Halmashauri hiyo haijawahi kutokea tangia kuanzishwa kwa Halmashauri hiyo kupata Soko la kisasa ambalo litapelekea Wajasiriamali kufanya biashara zao katika mazingira rafiki.
Kwa upande wa Mtendaji wa Kijiji cha Lituta Aisha Nyange akisoma taarifa ya ujenzi wa Soko hilo linalojumuisha matundu ya Vyoo 6,Guba na Vizimba amesema kijiji hicho kimeanza kutekeleza mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) awamu ya tatu mwaka 2015 ambapo utekelezaji wake ulifanyika kupitia Halmashauri ya Songea.
Nyange amesema Octoba 2022 Wananchi wa Kijiji cha Lituta walifanikiwa kuibua mradi wa ujenzi wa Soko na mchako wa makadirio ya bajeti ulifanyika kwa kwa kushirikiana na wataalamu ngazi ya Halmashauri na kupokea kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 190.
Amesema matarajio ya wananchi baada ya kupokea fedha za utekelezaji wa Mradi huo utakapo kamilika kupanua wigo wa bidhaa,kupunguza gharama kwa wananchi kwenda kutafuta mahitaji katika Wilaya za jira, Kuongeza mapato katika kijiji na Halmashauri.
“Tunatoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha kwaajili ya ujenzi wa Soko la kisasa katika Halmashauri yetu”.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Septemba 13,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa