WANANCHI Kata ya Matumbi kijiji cha Ifinga wamejiwekea benki tofari 400,000 kwaajili ya ujenzi wa miradi ya Serikali.
Mmwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Teofanes Mlelwa ametembelea Kata hiyo ya Matumbi Kijiji cha Ifinga na kukagua mradi wa benki tofari ulioanzishwa na wananchi.
Mlelwa amewapongeza Viongozi wa Kata na Kijiji hicho kwa kuanzisha mradi huo pamoja na wananchi wote.
“Sisi kama Halmashauri tunaleta fedha kwaajili ya ujenzi wa Miradi ,tuwapongeze wananchi wa Kijiji cha Ifinga jambo hili si jambo dogo uongozi mzuria huleta mambo mazuri”.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Matumbi Valentini Mtemauti amesema tofari hizo ni kwaajili ya maendeleo ya Kijiji ambayo Serikali inapoleta fedha miradi itekelezwe kwa wakati.
Mtemauti amesema Viongozi wamepanga kufyatua tofari laki 400,000 ,kupitia nguvu ya Kijiji wamechanga michango na kuweka wafanyakazi wanaofyatua tofari hizo katika upangaji wa tanuri inatumika nguvu kazi ya wananchi wenyewe.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Septemba 23,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa