HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba Imebainisha na kuandikisha wanafunzi 29 wenye Mahitaji Maalumu kwa mwaka wa Masomo 2022/2023.
Taarifa hizo imetolewa na Afisa Elimu Maalumu Halmashauri ya Madaba Teddy Sanga ofisini kwake mara baada ya kutembelea Shule za Msingi katika Halmashauri hiyo.
Sanga amesema hadi kufikia sasa wanafunzi waliobanishwa kuanzia darasa la awali hadi darasa la Saba katika Halmashauri hiyo wavulana 80 na wasichana 69 jumla ni 149.
“Mwaka 2022 wanafunzi wenye mahitaji maalumu waliofanya mtihani wa darasa la saba walikuwa 8 na wanafunzi 7 walifaulu na kuingia kidato cha kwanza Mwaka 2023 na mwanafunzi mmoja alifeli”.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Machi 3,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa