WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Lipupuma Kata ya Mkongotema Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wamefurahia kuanza kusoma katika Shule mpya.
Shule hiyo imejengwa kwa shilingi Milioni 331 kupitia mradi wa BOOST kwa jumla ya madarasa 8 ,jengo la utawala pamoja na madarasa mawili ya mfano ya awali.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohaed alipotembelea Shule hiyo wanafunzi walimshukuru kwa kusimamia ujenzi huo na kukamilika kwa asilimia 100.
Kutoka kitengo cha Mawasailiano Halmashauri ya Madaba
Novemba 20,2023
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa