HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba wameadhimisha wiki ya unywaji wa maziwa kwa kutoa elimu ya unywaji wa maziwa kwa wanafunzi 185 wa darasa la awali hadi darasa la pili shule ya msingi Ifugwa.
Wataalam wa idara ya kilimo mifugo na uvuvi wakishirikiana na Maafisa Lishe,ustawi wa jamii na idara ya Elimu msingi katika zoezi hilo wametoa elimu juu ya umuhimu wa unywaji wa maziwa kwa watoto.
Aidha maafisa hao wametoa wito kwa wazazi kuhakikisha zoezi la unywaji wa maziwa kwa watoto linakuwa endelevu ili kuhakikisha watoto hao wanakuwa na afya njema ambayo itapelekea kufanya vyema masomo yao wawapo shule.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Agosti 16,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa