UFUATILIAJI katika Shule za Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Madaba unaendelea katika kutambua uelewa wa wanafunzi.
Maafisa Elimu Halmashauri hiyo wametembelea Shule ya Msingi Igawisenga na Shule ya Msingi Turihani na kuwapima wanafunzi hao katika swala nzima la kusoma na kuandika.
Mara baada ya ukaguzi huo Afisa Elimu maalumu Teddy Sanga ametoa maagizo kwa walimu katika Shule hizo ikiwa ni pamoja na Wanafunzi kuimba nyimbo za kizalendo kwa ufasaha pamoja na kuwa na bebdi ya Shule.
“Naomba walimu muhakikishe mnaifahamu miradi ya Serikali inayotekelezwa katika Shule pamoja na kubainisha watoto wenye mahitaji maalumu”.
Afisa Elimu Kata ya Mkongotema Edwin Mlelwa amewapongeza walimu wa Shule hizo kuhakikisha mahudhurio ya wanafunzi wote wanakuwepo Shuleni kwa asilimia 100 kila siku.
Kutoka Kitengo cha Habari Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Machi 7,2023
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa