TIMU ya Maafisa Elimu wa Halmashauri ya Madaba imefanya kikao kazi na walimu Msingi na Sekondari pamoja na Maafisa Elimu Kata katika Kata 5 kwa lengo la kuweka mikakati ya Kitaifa ya uboreshaji wa Elimu.
Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Katika Halmashauri hiyo Saada Chwaya katika ziara hiyo ya kikao kazi amezungumza na Walimu wa Kata hizo ikiwemo Mtyangimbole,Ngumbiro,Mkongotema,Lituta na Mahanje kwa kuwajuza mikakati ya Kitaifa ya Elimu iliyowekwa kwaajili ya utekelezaji kuanzia Januari 2023 hadi Desemba 2023.
“Tumena matokeo ya Darasa la Nne,Darasa la Saba pamoja na Kidato cha Nne na tumeona wapi tulijikwaa ili mwaka huu 2023 tusijikwae tena “.
Chwaya ametoa rai kwa Walimu wahakikishe wanatekeleza mikakati iliyowekwa Kitaifa ili kuhakikisha Madaba inafanya vizuri kimkoa na Kitaifa kwa upande wa Elimu Msingi na Sekondari.
Teddy Sanga akisoma mikakati hiyo kwa Wakuu wa Shule Msingi na Sekondari amesema asilimia 100 kila mwalimu afanye tathimini ya matokeo ya upimaji wa maatokeo ya kitaifa ndani ya siku saba baada ya matokeo.
Amesema mikakati itakayo mwezesha kila mwalimu wa Sekondari na Msingi kufanya ufuatiliaji na tathimini ya ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi darasani kila mmoja na somo lake kwa majaribio ya wiki,mwezi,robo,robo tatu hadi mwaka kama wanapanda au wanashuka.
“Kila mwalimu wa Shule ya Msingi au Sekondari ahakikishe anampango kazi wa Utekelezaji na miongozo ya Kielimu ya Halmashauri na Shule kwa muhula wa kwanza wa masomo mpango kazi ndio dira”.
Hata hivyo Sanga amesema kwa upande wa Shule ya Msingi mwalimu ahakikishe asilimia ya mwanafunzi wa darasa la pili aweze kumudu stadi za kusoma afikapo Machi 30,kila mwaka kwa kusoma na kuheshabu.
Kwa upande wake Afisa utumishi wa Halmashauri hiyo Hope Challe amewakumbusha Walimu wajibu wao wawapo eneo la kazi pamoja na kuwachukulia wanafunzi ambao hawana uelewa wa haraka pamoja na kuto wanyanyapaa.
Challe amewakumbusha walimu kuepuka rushwa eidha kutoka kwa wazazi au watu wengine na kuwapelekea kupata changamoto ya kufukuzwa kazi, au kushushwa daraja pamoja na kufuata taratibu,miongozo na kanuni iliyowekwa na Serikali.
Afisa utumishi ametoa rai kwa walimu hao kuhakikisha wanawashirikisha wananchi miradi inayoletwa na Serikili na inayojengwa katika eneo lao ili wajue Serikali imeleta fedha kwaajili ya miradi ya maendeleo.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Januari 25,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa