WALIMU wa Awali na Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Mkoa wa Ruvuma wamepewa mafunzo ya Mitaala iliyoboreshwa.
Afisa Elimu Kata ya Mahanje Ruthness Mbuba akizungumza katika mafunzo hayo amesema lengo la kufanya mafunzo hayo kwa Walimu ni kuwajengea uwezo ili waweze kwenda na mabadiliko ya Mtaala ulioboreshwa wa mwaka 2023.
“Mtaala huu tunaanza kuutumia mwaka 2024 na unalenga darasa la awali,la kwanza na darasa la tatu na tunatarajia baada ya mafunzo haya walimu watatekeleza kwa kutumia mbinu mpya katika ufundishaji”.
Naye Afisa Elimu Elimu Maalumu Teddy Sanga akimwakilisha Afisa Elimu wa Halmashauri hiyo Saada Chwaya katika Mafunzo haya amesema katika mtaala huo walimu wasisahau watoto wenye mahitaji maalumu.
“Watoto wenye mahitaji maalumu siyo tu wale waliopo shuleni hata waliofichwa nyumbani walimu wenzangu tuwatumie viongozi wamaeneo hayo kama kuna watoto waliofikia umri wa kwenda shule lakini hawajaandikishwa waanze shule”.
Hata hivyo Sanga amewapongeza walimu katika Kata zote kwa kushiriki Mafunzo hayo ambayo yatasaidia kuboresha ufundishaji kwa watoto.
“Mafunzo haya yanakwenda kuboresha ufundishaji wetu kwa watoto ili tuweze kuendana na dunia ya Sayansi na Teknolojia kwa kupata vitu vipya na namna ya kuwafundisha”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmshauri ya Wilaya ya Madaba
Januari 11,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa