HALMASHAURI ya Madaba wametoa mafunzo kazi kwa walimu wakuu wa Shule za Msingi,taaluma na Maafisa Elimu Kata.
Akizungumza katika mafunzo hayo Afisa Elimu Msingi Edgar Dotto amesema Mwezi Septemba 2022 Halmashauri ya Madaba imeanza utekelezaji rasmi wa shuguli za MEWAKA.
“Leo tutajifunza mambo makubwa mawili la kwanza tutapitia utekelezaji wa MEWAKA katika vituo vyetu la pili tutaelekezana yale ambayo tuliyokuwa hatuyafahamu “.
Hata hivyo amesema wakati mpango wa MEWAKA unaanza kutekelezwa kuna makundi yalikuwa hayafahamu mpango wa MEWAKA ikiwa wakuu wa shule ni watekelezaji na Maafisa Elimu Kata ni wasimamizi.
Dotto amewapongeza Walimu kwa utekelezaji wa mpango huo kupitia uelewa mdogo wa MEWAKA na semina yaleo imesaidia kujifunza, na kuelewa kwa pamoja kupitia mada na mawasilisho yaliyotolewa.
“Siku chache zilizopita tulienda kufanya tathimini ya Taifa katka utekelezaji wa MEWAKA walipongeza kwa namna ambavyo tunatekeleza na tunatuma taarifa zetu isipokuwa maeneo machache”.
Mkuu wa Shule ya Msingi Mkwela Magreth Nyange ameeleza majukumu ya MEWAKA yanayotekelezwa katika shule,Kata na vituo vya walimu ikiwemo kuandaa mpango kazi,kuandaa mahitaji yaliyoandaliwa katika mpango kazi ya mafunzo kwa walimu,kuandaa bajeti ya uendeshaji,kuwaandaa wawezeshaji na washiriki wa mafunzo kwa walimu pamoja na kufanya tathimini ya mahitaji kabla ya kufanya mafunzo kwa walimu.
Nyange amese kwa upande wa Kata jukumu la kwanza ni kuandaa mpango kazi wa mafunzo kwa walimu ngazi ya Kata,kusimamia utekelezaji na mpango kazi na bajeti ,kuchambua na kujadili mahitaji yenye changamoto,kuaandaa mahitaji ya washiriki,kuchambua na kujadili maeneo yenye changamoto ngazi ya shule,kuandaa eneo la mafunzo,kuandaa washiriki, kuandaa ratiba ya kituo,pamoja na kuandaa mahitaji ya washiriki.
Kwa upande wake Mthibiti ubora wa Shule Halmashauri ya Madaba Godlove Makongwa amesema majukumu ya MEWAKA kuandaa mahitaji ya walimu pamoja na kuangalia umahili wa Mwalimu, kupokea taarifa ngazi ya Kata ili ngazi ya shule waweze kuandaa mahitaji yanayohitajika na kuwasilisha katika Kata.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka :Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Madaba
Februari 8,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa