TAASISI ya kuthibiti ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI) iliyopo chini ya Wizara ya Kilimo imetoa mafunzo kwa wakulima wa mbegu bora za maharage kwa wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Mkoa wa Ruvuma na Wakulima wa Halmashauri ya Ludewa Mkoa wa Njombe.
Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Amani Kata ya Lituta Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kwa siku mbili Desemba 13,2022 hadi Desemba 14,2022.
Akizungumza katika mafunzo hayo Mkaguzi wa Mbegu kutoka TOSCI Kanda za Nyanda za Juu Kusini Frenk Mwilenga amesema TOSCI ilianzishwa kwa mujibu wa sheria namba 18 ya mbegu ya mwaka 2003 ili kuendeleza majukumu ya TOSCA iliyoanzishwa mwaka 1973.
“Kama tunavyojua ubora wa mbegu upo chini na tulikuwa tunatoa mafunzo mara kwa mara ili kuhakikisha wakulima wa Madaba wanazalisha mbegu bora za Maharage”.
Hata hivyo amesema mara baada ya mafunzo hayo kwa wakulima watapewa vyeti vitakavyowawezesha kuzalisha mbegu bora katika Halmashauri ya Madaba na itawasaidia wakulima kujipatia mbegu kwa urahisi.
Kwaupande wake Afisa mauzo kutoka kampuni ya Mtewele Jeneral traders Benedict Mgaya amesema kwa kushirikiana na watu wa Britain na TOSCI kwaajili ya kutoa mafunzo ya uzalishaji wa Mbegu bora za Maharage ikiwa na lengo la kuongeza thamani zao hilo.
Amesema Lengo kuwakutanisha wakulima baada ya mafunzo hayo begu zitakazozalishwa zitanunuliwa na Kampuni ya Mtewele pamoja na vikundi na wadau wengine.
Moja kati ya washiriki wa mafunzo hayo Yusta Mahuwi kutoka kijiji cha Mwande Kata ya Matetereka Halmashauri ya Madaba amewashukuru Taasisi na Kampuni kwa kuwafikilia na kuwapatia mafunzo hayo ikiwa itasaididi kilimo cha zao la Maharage kulima kwa tija.
Mahuwi amesema kilimo hicho kilikuwa kinalimwa kwa mazoea na kuvuna kwa heka gunia 3 badala ya kupata mafunzo hayo kutoka kwa wataalamu wanatalajia kuvuna zaidi ya gunia 8 kwa heka.
“Mwanzoni tukilima tulikuwa tunavuna na gunia 3 kwa heka kwasababu tulikuwa tunalima kwa mazoea,natulikuwa tunaona tumepata sana na mbege tuliyokuwa tunatumia ilikuwa za mda mrefu tangia enzi za mababu zetu”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Desemba 13,2022.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa