KAIMU MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Pololeti Mgema amefungua Semina inayolenga kuongeza Uelewa wa Matumizi ya Vipimo sahihi Ruvuma.
Akizungumza katika Semina hiyo amesema ni semina iliyolenga makundi mbalimbali ikiwemo Wakulima,Wajasiliamali,Viongozi wa Masoko,Wasindikaji wa Unga,na wafanyabiaashara wa Jumla.
“Natoa shukrani zangu za pekee kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kujenga mazingira bora ya ufanyaji wa Biashara ya Mazao na kuendelea kusisitiza utumiaji wa Vipimo sahihi ili kuleta tija na usawa kwa Mkulima ”.
Hata hivyo Mgema amesema ni mwendelezo wa utekelezaji wa Wakala wa Vipimo kwa jamii na kutoa Elimu kwa wadau kupitia Television(TV)Magazeti,Radio pamoja na Mikutano mbalimbali.
Amesema kumekuwa na matumizi makubwa ya Vipimo batili katika maeneo ya Biasharahususani kwenye Masoko ya Manispaa na Wilaya na watu wamekuwa wakitumia Vipimo visivyo rasmi vinavyojulikana kama makopo,dumla,ndoo na lita.
“Katika Ilani yetu ya CCM ya chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 ibara ya 37B(d,f,g,h) ina sisitiza uongezaji wa tija na faida katika shughuli za wakulima ili kuongeza uzalishaji”.
Pia Mgema ameipongeza Taasisi ya Wakala wa Vipimo kwa kuanzisha maeneo mapya ya ukaguzi ilikupanua wigo wa kumlinda mlaji kutokana na matumizi sahihi ya Vipimimo.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Vipimo Nyagabona Mkanjabi katika semina hiyo amesema kwa Mkoa wa Ruvuma matumizi ya Vipimo sahihi yapo china sana kwa wafanyabiashara ishara inayoonesha bado hawajahamasika kutumia vipimo sahihi.
Mkanjabi amewaomba wafanyabiashara kuanza kutumia ili wanchi wafuate matumizi ya makopo siyo sahihi
“Wafanyabiashara kutumia makopo na kuamini jamii haikubari bado siyo sahihi kwa sababu hao wanaolalamika wanaenda Buchani ananunua nyama inayopimwa kwenye mzani,Sukari ananunua kwa kupimwa kwenye mzani ni utamaduni ambao watu wamejijengea pamoja na wateja wao kutumia makopo kwa namna nyingine wanajinufaisha wafanyabiashara na kuwapunja wateja”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa habari Halmashauri ya Madaba
Mei 5 ,2021
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa