HAKIM Mkazi Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Rita Chale ametoa elimu ya Mirathi katika maadhimisho ya siku ya wajane yaliyofanyika Juni 27,2024.
Akizungumza katika maadhimisho hayo amesema mirathi inahusisha mali za marehemu na usimamizi ikiwaenzi za uhai wake alikuwa na mali na ameacha ndugu ,watoto na mke/mume.
Amesema Mirathi inayoongozwa na sheria za kimila au kidini kutokana na mali alizoacha marehemu kwa warithi wa kwanza ambao ni muke/mume na watoto
Chale amesema baada ya marehemu kufa familia inaweza kupendekeza mtu wa kusimamia mirathi na mahakama kumtea kwa kuangalia vigezo ambavyo wameona au kumkataa kwa sababu walizoona.
“Tuelewe kitu kimoja msimamizi wa mirathi siyo mrithi kazi yake ni kusimamia mali zilizokuwa na mmiliki na akafariki”.
Hata hivyo amesema katika ugawaji wa mali za mirathi mahakama haina mamlaka ya kugawa mali bali familia igawane kwa kiasi gani kwa kila mmoja hapo familia zitagawa kwa mtindo wa kimira na kidini.
“Tunashauri sana watu wakae kama familia hata yeye aliyeacha mali hakutaka mali zake ziwe chanzo cha ugomvi angetambua ni hivyo mali zake angeuza kabla hajafa ”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashuri ya Wilaya ya Madaba
Juni 27,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa