WAHITIMU wa chuo cha Sauti Songea wa Mwaka 2016 hadi 2018 wafani tofauti wametembelea eneo la Uwekezaji la Silver Land Ndolela Katika Halmashauri ya Madaba wameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile na Mkuu wa Idara ya Kilimo,Ufugaji na Uvuvi Joseph Mrimi Halmashauri ya Madaba.
Moja kati ya wahitimu hao Ernest Anord amesema wemepewa fursa ya kufika kujifunza katika eneo la uwekezaji wa mbegu za mazao mbalimbali na Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile.
Anord amesema wameona faida ya kufika katika eneo la Hekta 500 linalowekeza uwekezaji mkubwa wa mbegu za viazi mviringo, Alizeti na Maharage aina 72 za Mbegu,Ngano kupitia umwagiliaji teknolojia ya kisasa.
Meneja wa Kampuni hiyo ya Silver Land Ndolela Christian Kihindo amesema Kampuni hiyo kwa mara ya kwanza walianzaza kulima Mahindi ya chakula,ngano pamoja na Soya walilima Mwaka 2016/2017 hawakufanya vizuri walibadilisha na kuanza kulima mbegu.
Kihindo amesema kwasasa wawekezaji hao Mbegu zinazozalishwa wanawauzia makampuni ya hapa Tanzania kama vile Seed co,Baya pamoja na Zamseed na Maharage yanauzwa Nchi ya Italy.
Hata hivyo Meneja amesema mbegu za Alizeti zinazalishwa kwaajili ya wakulima wa Tanzania pamoja na shirika la Kiserikali ASA.
Amesema wawekezaji hao wanalima mara 2 kwa mwaka kwa umwagiliaji kupitia umeme wao uliotegwa kupitia maporomoko ya mto Luhuhu umeme unaotumika ni asilimia 80 na Umeme wa Tanesco asilimia 20.
Kihindo amesema katika Kampuni ya Silver Land Ndolela kuna wafanyakazi 150 walioajiliwa na ajira ya kudumu na wafanyakazi wa mda mfupi zaidi ya 600 wanaokuwa kwa msimu.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Septemba 22,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa