MKUU wa Wilaya ya Songea Pololeth Mgema amewaagiza wananchi wa Halmashauri ya Madaba kuwachukulia hatua wanao halibu misitu.
Hayo amezungumza alipo tembelea kijiji cha Lilondo na kushiriki zoezi la upandaji wa miti katika eneo la Shule ya Sekondari Lilondo.
“Misitu ni uhai wetu tuwachukie wanaoharibu misitu kwenye vikao vya hadhara vijijini iweajenda ya kudumu “.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Teofanes Mlelwa amewapongeza wananchi wa Kata hiyo kwa kuhamasika katika zoezi la upandaji wa miti na kutambua umuhimu wa upandaji wa Miti.
Amesema wananchi hao waendelee kuwa na moyo wa kujitoa ikiwa leo nisiku ya kwanza ya mwezi wa kwanza Januari 2023 lakini imekuwa jambo jema wananchi hao kutambua umuhimu wa kupanda miti.
Kwa upande wake Meneja wa Shamba la Miti Wino Grory Kassimir amesema ni siku ya uzinduzi wa upandaji miti katika kijiji cha Liliondo katika siku 2 imepandwa miti 1,000 na miti 100,000 ya kibiashara watapewa wananchi.
Mhifadhi ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha kila mwananchi anapanda miti na kuitunza na amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa kujumuika katika zoezi hilo muhimu.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Madaba
Januari 1,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa