KITUO cha afya Matetereka Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kilichojengwa kwa zaidi ya shilingi bilioni moja kimeanza kutoa huduma.
Hayo amesema mganga Mfawidhi wa kituo hicho Yusuph Mnazi katika ziara ya Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama kuwa hadi kufikia sasa wagonjwa 275 wamepata huduma katika kituo hicho,wagonjwa wa marudio 380,wanawake wajawazito 10,huduma ya uzazi wa mpango kwa akinamama na akina baba 27.
“Serikali imeleta vifaa tiba ambavyo mda si mrefu vitaanza kutumika na huduma itakayopatikana itakuwa ni bora na bobezi”.
Diwani wa Kata hiyo Hamfrey Mwenda amesema ujenzi wa Kituo hicho cha afya Matetereka kilijengwa kwa shilingi milioni 562 kwa mradi wa tozo mwaka 2021/2022 Milioni 500 ililetwa kwa awamu ya mbili,na mapato ya ndani ya Halmashauri ilitoa kiasi cha shilingi Milioni 62 kwa awamu mbili tofauti ikiwa Mwaka 2022/2023 ilitoa Milioni 42, Mwaka 2023/2024 ilitoa milioni 20.
Hata hivyo ujenzi huo unahusisha majengo manne OPD,mama na mtoto, maabara na jengo la kufulia pamoja na kichomea taka majengo hayo yamefikia hatua ya ukamilishaji na kuanza kutoa huduma.
Mwenda ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama kwa kuleta fedha kwaajili ya ujenzi wa Kituo cha afya.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Julai 15,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa