WAGANGA wa Tiba za asili Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wamepewa mafunzo ya kuzingatia miiko na maadili ya utoaji huduma kwa wagonjwa.
Mafunzo hayo yametolewa na Mratibu wa tiba asili na mbadala Shani Kabuga ,Afisa Lishe John Mapunda pamoja na Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma Methew Mihangwa katika ukumbi wa Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba.
Mihangwa ameeleza kuwa Mganga wa tiba za asili endapo atapata dalili za ugonjwa wa TB anapaswa kuwahishwa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya mara moja.
Mratibu wa Kifua kikuu na Ukoma ameeleza dalili hizo ikiwa ni pamoja na Mgonjwa kutokwa na Jasho jingi usiku, kukohoa sana zaidi ya siku saba,homa za mara kwa mara,vikohozi vilivyochanganyika na damu pamoja na maumivu ya mifupa.
Kwa upande wake Mratibu wa tiza za asili na tiba mbadala Shani Abdul Kabuga amesema kanuni taratibu na sheria za waganga wa asili na mbadala,kanuni zinazosimamia utekelezaji wa sheria na 23 ya 2002,adhabu za kisheria kwa mganga au msaidizi wa tiba za asili anayetoa huduma kinyume na sheri pamoja na mambo yote yaliyokatazwa katika tiba za asili.
Afisa Lishe Halmashauri ya Madaba John Mapunda katika mafunzo hayo ya waganga wa tiba asili na mbadala amehimiza kuhakikisha wanawatambua wateja wenye utapiamlo na kuwashauri kwenda kwenye vituo vya huduma ya Afya badala ya kuendelea kuwaweka katika maeneo yao ya matibabu jambo ambalo linaweza kuhatarisha maisha mfano kwashakoo,unyafuzi,pamoja na upungufu wa Damu.
Imeanadaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Septemba 26,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa