Msimamizi mkuu wa uchaguzi Sajidu Idrisa Mohamed akiwakilishwa na msimamizi msaidizi wa uchaguzi Abdul Manga ametoa rai kwa waandikishaji wa daftari la wapiga kura kulichukulia uzito wake zoezi la uandikishaji wa daftari la wapiga kula.
Hayo amesema katika mafunzo ya waandikishaji wa daftari la mpiga kula yaliyofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Madaba day amesema Serikali inatumia fedha nyingi kwaajili ya uchaguzi.
Hata hivyo amesema amewaomba kutambua kwa wao ni watumishi waumma wajue sheria,taratibu na kanuni ikiwa watu wa ofisi ya Rais Tamisemi waliamua kuweka vigezo zoezi hilo lifanywe na watumishi wa umma”.
“Mimi kama msimamizi ngazi ya Wilaya sitapenda kuona dosari yoyote inatokea kwa mmoja wetu wakati wa kutekeleza zoezi hili na nina imani mnayajua vema maeneo yenu mkafanye kwa weledi na uzalendo mkubwa “.
Hata hivyo amesema waandikishaji hao wahakikishe wanatunza vifaa vyote vitakavyotumika katika zoezi hilo.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano
Oktoba 7,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa