VITENDO vya ukatili wa kijinsia 442 vimeripotiwa katika Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma katika kipindi cha miezi sita iliyopita .
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas wakati anatoa taarifa kwa wanahabari kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia nchini Ikulu Ndogo mjini Songea.
Amesema kati ya vitendo hivyo kubaka matukio 24,kujeruhi matukio 48,mimba kwa wanafunzi matukio 49,matukio 112 ya kudhuru mwili,shambulio la aibu matukio 45 na kutumia lugha za matusi matukio 42.
RC Thomas amelitaja lengo la maadhimisho hayo ambayo hufanyika kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 10 kila mwaka ni kujitathimini katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia. “Katika kipindi hiki kila mwananchi atapata fursa kutafakari masuala ya ukatili wa kijinsia na hatimaye kama Jamii kukata shauri ili kutokomeza vitendo hivyo “,alisisitiza.
Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa jamii nzima vikiwemo vyombo vya habari kutoa elimu endelevu ili kunusuru jamii dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Kanali Thomas ameutaja wajibu wa vyombo vya haki kama polisi na mahakama kuwa ni kusimamia sheria na kutoa elimu ya sheria kwa kila aina ya ukatili.Kaulimbiu ya maadhimisho kwa mwaka 2022 ni kila uhai una thamani:tokomeza mauaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma.Novemba 26,2022
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa