HALMASHAURI ya Madaba wamesisitizwa kuendeleza mahusiano mazuri katika utendaji Kazi baina ya Madiwani na watumishi.
Hayo amesema mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Amandus Chilumba katika Baraza la Madiwani katika kikao cha robo ya tatu mwaka 2023/2024.
“Hizi Halmashauri sawa na sarafu ambazo zinategemeana hakuna upande mwingine ni bora kuliko upande wa mwenzake Madiwani hamuwezi kufanya kazi bila wataalam na wataalam hamuwezi kufanya kazi bila madiwani”.
Hata hivyo chilumba amempongeza Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwa kuhakikisha anamaliza migogoro na kuweka mikakati ya pamoja.
CHilumba ametoa rai kwa madiwani na wataalam kuhakikisha wanabuni vyanzo vipya vya mapato na kusimamia vile ambavyo vipo.
“Mara nyingi nasisitiza wataalam na Madiwani tuibue vyanzo vipya na tusimamie hatuwezi kusimamia wananchi bila kuwa na vyanzo vingi vya mapato tunataka tuone hivyo”.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Teofanes Mlelwa amesema kutokana na swala la ukusanyaji wa mapato wamejipanga kuhakikisha wanasimamia ikiwa bila mapato Halmashauri haitakuwa na maendeleo.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
April 30,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa