Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Mussa Rashid amewapongeza Madaktari bingwa Bobezi wa Mama Samia kwa kuwa chuo cha kujifunza kwa Madaktari wa halmashauri ya Madaba.
Hayo amesema leo alipowatamburisha madaktari hao kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kuwa ujio wao umeleta tija kupitia uwekezaji ambao Rais Samia ameufanya kwa mara ya pili.
“Ni mpango endelevu kwa Nchi yetu hii ni awamu ya pili sasa awamu ya kwanza ilikuwa mwezi wa tano mwaka huu 2024”.
Hata hivyo Rashid amesema mpango huu wa kuleta Madaktari bingwa umeleta chachu kwa wataalam wa Afya kupenda kujiendeleza kusoma na ikiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameleta vifaa ambavyo vinahitaji utaalam katika matumizi yake.
“Jambo hili kwa wananchi limekuwa ni heri sana limepunguza gharama kubwa kufuata huduma Muhimbili na sehemu zingine huu mpango ni mzuri tunampongeza Rais kwa kuleta huu utaratibu na kufanya Nchi iweze kufikika kwa haraka kupitia Afya“.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Oktoba 30,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa