HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba imepokea Fedha kiasi cha Shilingi Milioni 128 kutoka Serikali kuu kwaajili ya ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalumu shule ya msingi Madaba.
Mkuu wa Shule hiyo Victor Luoga akisoma taarifa ya ujezni wa bweni hilo kwa Kamati ya Fedha inayoongozwa na mwenyekiti wa Halmashauri Teofanes Mlelwa amesema ujenzi huo umeanza tarehe 13,Mwezi 10 na kutarajia kukamilika Disemba 30,2023 na kuanza kutumika.
Mkuu wa Shule amesema hadi kufikia sasa ujenzi umefikia hatua ya ringibim upande mmoja na kumwaga jamvi.
Luoga ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha za ujenzi wa Bweni ambalo litawasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu kukaa karibu na eneo la Shule
Kutoka Kitengo cha Mawsiliano Halmashauri ya Madaba
Novemba 7,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa