TIMU ya wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma iliyoongozwa na Katibu tawala Msaididi Miundombinu Gilbert Simya wametembelea na kukagua Miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Moja ya mradi uliokaguliwa ni ujenzi wa Soko (Vizimba 84) matundu 6 ya vyoo na Guba unaotekelezwa kwa shilingi Milioni 190 katika Kijiji cha Lituta Kata ya Lituta.
Mradi huo umefikia hatua ya kufunga boksi kwaajili ya Lenta guba na vyoo hatua ya kupandisha kuta.
Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Hancepopo Wayotile amesema hadi kufikia sasa wametumia zaidi ya shilingi Milioni 54 na mradi unajengwa kwa mda wa miezi sita umeanza Septemba 2023,na kukamilika Februari 12,2024.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Novemba 16,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa