MSIMAMIZI Mkuu wa Uchaguzi Jimbo la Madaba Mkoa wa Ruvuma Shafi Kassim Mpenda amemtangaza Mbunge Joseph Kizito kupita bila kupingwa ikiwa ni mara ya pili katika Jimbo hilo.
Akitoa taarifa hiyo ofisini kwake jana amesema Jimbo la madaba uchaguzi umefanyika kwa utulivu kabla ya zoezi hilo kata nne Madiwani wamepita bila kupingwa na kata nne Madiwani wamepita kwa kuchaguliwa kwa chama cha CCM.
Hata hivyo amesema Jimbo la Madaba wamefanikiwa kufanya uchaguzi katika kata nne na vituo vya kupigia kura vilikuwa miamoja na nanae na hali ilikuwa shwali.
“Kwa upande wa Ubunge Mh. Joseph Kiziti alifanikiwa kupita bila kupingwa katika hatua za awali za uteuzi katika nafasi ya udiwani kata zilipita bila kupingwa na kata nne tulifanya uchaguzi ikiwa ya Kata ya Mtwangimbole ameingia diwani mpya wa CCM na kumwacha mbali Diwani wa Chama cha Demokrasia na Maendelea ya Jamii (CHADEMA) na kuibuka kidedea kwa kura nyingi katika ngazi ya chama cha CCM’’.amesema Mpenda.
Mpenda amesema ikiwa ni mara yake ya kwanza kuteuliwa kusimamia uchaguzi amemkabidhi Mbunge wa Jimbo la Madaba Cheti na kusubilia kuapishwa rasmi.
Mpenda amewapongeza Maafisa uchaguzi kwa ushirikiano waliouonyesha katika kipindi chote cha uchaguzi kwa ufuatiliaji katika vituo vyote na kuhakikisha zoezi hilo limefanyika na kuisha salama.
Kwa upande wake Mh. Diwani mteule wa kata ya Lituta Jimbo la Madaba Orasmo Pili aliyeteuliwa kwa chama cha CCM amewashukuru wananchi kwa kumchagua na ameahidi kusimamia Maendeleo na kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi CCM na kuonyesha ushirikiano kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Madaba.
Naye Mh. Diwani aliyepita bila kupingwa katika chama cha CCM Vastusi Mfikwa Kata ya Mkongotema Jimbo la Madaba amesema amepita bila kupingwa kutokana na wananchi wamemwamini na utekelezaji wake akishirikiana na viongozi wa Ngazi ya Juu.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Madaba
Oktoba 29,2020.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa