UFUATILIAJI wa ufundishaji na upimaji wa wanafunzi katika Shule za Msingi Halmashauri ya Madaba unaendelea kwa mda wa miezi miwili kuanzia shule zilipofunguliwa Januari 9,2023.
Maafisa Elimu Msingi Katika Halmashauri hiyo wametembelea Shule mbili za Msingi Mkwera na Madaba na kuangalia uelewa wa wanafunzi wa Darasa la awali hadi la nne kama wanamudu kusoma na kuandika.
Afisa Elimu Takwimu na Vifaa Raphael kibirigi amewakumbusha Wlimu wajibu wao wanapokuwa katika eneo lao la kazi ili kuhakikisha wanafunzi wanamudu kusoma pamoja majukumu mengine.
Kibirigi ametoa rai kwa walimu hao kuhakikisha wanashirikiana na Mwalimu Mkuu kusimamia miradi inayoletwa katika Shule husika ukiwemo mradi wa Nyumba moja ya mwalimu katika Shule ya Msingi Madaba na miradi mingine ambayo hivi punde itaanza kutekelezwa ikiwemo ya Swash na Boost.
“ Walimu hakikisheni mazingira ya Shule yanakuwa safi hasa katika kipindi hiki cha mvua na madarasani”.
Mkuu wa Shule ya Msingi Mkwera Magreth Nyange amesema uandikishaji wa wanafunzi wa awali mwaka 2023 hadi kufikia sasa waliopo darasani ni 111 na darasa la kwanza 87 na kufikia kiwango cha kuvuka lengo.
Hata hivyo Shule ya Msingi Madaba mpaka kufikia sasa wanafunzi wa darasa la awali wapo 101 na darasa la kwanza 98.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Madaba
Machi 1,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa