Wakala wa Misitu Wino (TFS) wametoa mifuko 200 ya Saruji katika shule ya Sekondari Wilima Halmashauri ya Madaba kwaajili ya ukarabati wa Madarasa ya Kidato cha tano na sita
Hayo ameyasema Meneje wa TFS Wino Grory Fotunatus aliyekuwa Mgeni rasmi katika Mahafari ya 34 ya Kidato cha nne mwaka 2023 akiwakilishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Madaba Teofanes Mlelwa.
Mkuu wa Shule hiyo Christopher Mng’ong’o akisoma taarifa katika hafla hiyo amesema shule hiyo ni ya wananchi wa Halmashauri ya Madaba na inapokea wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali za Nchi ya Tanzania.
Mng’ong’o amsema shule hiyo inamajengo ya kutosha, na wallimu 15,wanafunzi wanafanya vizuri mihihani na kufauru ikiwa mwaka 2022 wanafunzi waliohitimu kidato cha nne wote walifaikiwa kuingia kidato cha tano na kidato cha Sita walifanikiwa kujiunga na vyuo mbalimbali.
Amesema Shule hiyo imepata wahisani mbalimbali wakiwemo umoja wa wanafunzi waliosoma Wilima wamejenga madarasa mawili ya kidato cha tano na sita,Wino SACCOS wamenunua vitabu,TFS wamesaidia mbegu za miti pamoja na viriba vya kupandia miti,Mbuge wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama amekarabati maabara .
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoa kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Oktoba 14,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa