Wakala wa misitu Tanzania TFS wameunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 39 katika taasisi za kidini na Serikali.
Muhifadhi Mkuu wa shamba la miti Wino Grory Fotunatus Halmashauri ya Wilaya ya Madaba akizungumza katika makabidhiano ya vifaa hivyo kwa mbunge wa Jimbo la Madaba Mhe.Joseph Mhagama amesema lengo la taasisi hiyo ni kuunga mkono kwa wananchi walipofikia ili taasisi hiyo iweze kumalizia
“Tumekuja mahali hapa tunaunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha juhudi za wananchi pale walipofikia na sisi tunaunga mkono ili waweze kuhifadhi misitu vizuri”.
Aidha muhifadhi amemshukuru Mhe.Mbunge kwa kuendelea kutoa ushirkiano na kuunga mkono jitihada za wananchi na kuwakumbusha katika eneo la uhifadhi wa misitu.
“Msitu wa wino umezungukwa na vijiji vingi na kunawananchi hapa madaba wanamashamba kule ndiomana tumekuja kuunga mkono”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Julai 19,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa