AGNES Mgimba ni mkazi wa Kijiji cha Kipingo Kata ya Lituta ni mnufaika wa mpango wa TASAF kwa mda wa zaidi ya miaka mitano.
Afisa maendeleo ya Jamii Juma Komba Halmashauri ya Madaba ametembelea Kaya hizo na kuangalia jinsi mnufaika huyo alivyojiwekeza katika ufugaji na kuepukana na umaskini.
Mgimba amesema TASAF imemsaidia kwa kusomesha watoto ikiwemo mmoja kufika chuo kikuu na wawili kumaliza kidato cha nne, pamoja na kuwa na chakula cha kutosha na familia kuwa na furaha ya maisha.
“Mpango wa TASAF kabla haujaanza nilikuwa na hali duni sana,nimesomesha wanangu,nilikuwa sina chakula kwa sasa ninachakula cha kutosha,nina maji pamoja na umeme na ufugaji wa kuku na hii ni awamu ya pili sasa na fuga na nilipata faida ya laki tano”.
Hata hivyo mama Mgimba amempongeza Rais wajamhuri ya muungano wa Tanzania Rais Samia kwa kuhakikisha TASAF inawasaidia watu Maskini na kuondokana na hali ngumu ya Maisha.
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mimi nashururu sana kwa kuangalia watu wa hali ya chini nilikuwa nalazwa mara kwa mara nilikuwa na mawazo mengi ,nilitelekezwa na mumewangu zaidi ya miaka 10 watoto wakiwa wadogo”.
Kwa upande wake Mnufaika wa TASAF Selina Kisite kutoka Kijiji cha Ifugwa ameelezea namna ambavyo Mpango wa TASAF ulivyomnufaisha mara baada ya kuachwa na Mume wake zaidi ya miaka 15.
Amesema Mpango wa TASAF Ulimsaidia kusomesha watoto pamoja na ufungaji wa Mbuzi zaidi ya 10,Kuku zaidi ya 20 pamoja na ujenzi wa nyumba ya kuishi na kuepukana na Nymba za kupanga.
Kisite ameeleza namna ambavyo kupitia hela hizo za TASAF licha ya kufuga mifugo mbalimbali alikuwa analima bustani ya mbogamboga nakumsaidia kupata kipato zaidi na kupelekea maisha yake kuwa mazuri.
“Mimi nilikwa nikipokea hela kutoka TASAF nilikuwa nagawa katika kilimo cha bustani,Ufugaji wa Kuku na Mbuzi ikanipelekea kujenga nyumba yangu na kuepuka na Nyumba za kupanga miaka mingi baada ya kuachana na mume wangu”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Habari Halmashauri ya Madaba
Novemba 29,2022.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa