WANANCHI wa Halmashauri ya Madaba walioingia katika Mfumo wa TASAF wamenufaika na kuondokana na Umasikini.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri hiyo Juma Komba ametembelea kaya mbalimbali za walengwa wa TASAF na kuangalia maendeleo ya wananchi hao mara baada ya kuingia kwenye mfumo huo kwa zaidi ya miaka mitano na kuona matokeo chanya kwa Juma Bonifance anayepatikana katika Kata ya Lituta Kijiji cha Kipingo.
Afisa maendeleo amejionea kwa mlengwa huyo kuondokana na hali duni kutoka kuishi katika nyumba ya Nyasi na kujenga Nyumba nzuri ya Kuishi pamoja na kusomesha watoto,na kuwa na miradi mbalimbali ya kilimo pamoja na ufugaji.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa