HALMASHAURI ya Madaba imetekeleza miradi mitatu ikiwemo barabara zimekamilika kwa asilimia 100 na mradi wa maendeleo chini ya mfuko wa fedha za barabara umetekelezwa kwa asilimia 94.
Akitoa taarifa hiyo Mhandisi Shabani Ally Kasanzu amesema hali ya barabara katika halmashauri ya madaba imegawanyika katika makundi makuu manne ambapo jumla ya kilomita 31.74 ni barabara za changarawe,kilomita 1.7 Lami,kilomita 593.76 ni barabara za udongo na kilomita 2.5 barabara za nzege.
Kasanzu amesema Wakala wa barabara Vijijini(TARURA) Halmashauri ya Madaba inamtandao wa barabara ya kilomita 629.70 katika hizo kilomita 196.31 ni za mjazo (Feeder Road),399.28 ni za Mkusanyo (Collection Roads)na kilometa 34.11ni za jamii au Kijiji (Community Roads).
Mhandisi amesema miradi inayotekelezwa chini ya mfuko wa fedha za Barabara ni Barabara ya Lutukila,Magingo,Barabara ya Madaba Lita,Magingo-Kipingo yenye kilomita 7 na matengenezo ya sehemu kolofi kazi imekamilika kwa asilimia 85.
Barabara ya Wino –Ifinga –Luhuji na Madaba ,Maweso,Lukumbulu matengenezo ya Mda maalumu yenye kilimita 15, kazi imekamilika kwa asilimia 100.
Amesema miradi ya maendeleo inayotekelezwa chini ya mfuko wa fedha za Barabara ya Ifinga,Luhuji,kiwango cha changarawe (DEVO under Road Fund) yenye kilomita 15 imefikia asilimia 94 na kazi bado inaendelea.
“Wakala wa Barabara Vijijini TARURA Halmashauri ya Madaba inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufinyu wa bajeti,inayoidhinishwa ukilingana na mtandao halisi wa jiografia,Magari yenye uzito mkubwa kupita kwenye barabara zilizochini ya wakala,na wananchi kuendesha shughuli za kilimo katika maeneo ya hifadhi ya barabara kuziba mifereji iliyochimbwa”.
Amesema utatuzi wa changamoto hizo wameendelea kuishauri serikali ili kupanua uwigo wa ukomo wa bajeti ya matengenezo ya barabara ikiwa ni pamoja na kutafuta vyanzo vingine vya fedha na kutoa elimu kwa viongozi wa Kata na vijiji kuhusu sheria na kanuni za barabara zinazosimamia matumizi na usimamizi wa barabara.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa habari Halmashauri ya Madaba
Januari 29,2021
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa