HALMASHAURI ya Madaba imeandikisha Wakulima 20,336 kwaajili ya zoezi la ununuzi wa mbolea ya Ruzuku hadi kufikia sasa wakulima waliosajiliwa kwa alama za vidole ni 12,881.
Hayo amesema afisa Pembejeo wa Halmashauri hiyo Thadei Mbele mara baada ya kutembelea vituo vya ununuzi wa mbolea za Ruzuku 9 vilivyopo katika Maeneo mbalimbali ya Halmashauri na kati ya Mawakala hao watatu wameanza kuuza mbolea hizo ikiwa ni Mtewele General Traders Madaba Ndelenyuma,Damiani Myoka Madaba pamoja na Devota Njawike Madaba.
“Jumla ya Mawakala 9 wamepata nafasi ya kuwahudumia wakulima kwa kuwauzia mbolea ya ruzuku kwa msimu wa kilimo 2022/2023”.
Mbele amesema hadi kufikia sasa Mbolea za Ruzuku zilizoingia katika Halmashauri hiyo Jumla ya Tani zote ni 443 ikiwemo DAP tani 47,MINJINGU PLUS tani 3, MINJINGU TOP DRESSING tani 1,SA tani 115,CAN tani 50.5,UREA tani 194.5,YARAMILA AMIDAS tani 32.
Afisa kilimo ameelezea baadhi ya changmoto zilizojitokeza kwa wakulima waliosajiliwa na kupata namba,kutopata huduma kutokana na kuingiliana kwa namba za wakulima na kutoonekana namba kwenye mfumo.
“Wakulima waliopata changamoto Suluhisho la changamoto hizi waje katika idara ya Kilimo,Mifugo ,na Uvuvi katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri”.
Amesema changamoto nyingine ni baadhi ya Mawakala wengi waliopata Lesen za Kuuza Mbolea za Ruzuku toka mamlaka kushindwa kuingia katika biashara ya kuuza Mbolea za Ruzuku kutokana na mitaji midogo.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Madaba
Novemba 16,2022.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa