• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

TANGAWIZI yawaingizia wakulima wa Madaba zaidi ya bilioni moja

Posted on: December 7th, 2020

WAKULIMA wa Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma wamepata zaidi ya shilingi bilioni moja kutokana na mauzo ya zao la tangawizi katika kipindi cha mwaka 2019/2020.

Afisa Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri hiyo Joseph Mrimi akizungumza ofisini kwake mjini Madaba,amesema kutokana na mauzo hayo  Halmashauri imeingiza zaidi ya shilingi milioni 16 ambazo ni mapato ya ushuru sawa na asilimia tatu ya mapato .

Mrimi amesema uzalishaji wa tangawizi katika Halmashauri hiyo msimu huu umefikia tani 5,117 ambazo zimeuzwa  ndani na nje ya Nchi.

“Halmashauri ya Wilaya ya Madaba tumeweka mkakati wa kuongeza  thamani ya zao hilo na kuongeza uzalishaji zaidi wa zao hilo ambalo soko lake hivi sasa ni kubwa’’,alisisitiza Mrilimi.

Amesema Halmashauri imetenga jumla ya Hekari 400 kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda mbalimbali vya kuchakata mazao ya kilimo ikiwemo zao la tangawizi.

Kwa upande wake Mchumi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Bosko Mwingira amesema,Halmashauri ya Wilaya hiyo imechukua hatua mbalimbali za kulitangaza zao hilo  katika maonesho ya wakulima nanenane Kanda ya Mbeya na Maonesho  ya Uwekezaji katika Mkoa wa Ruvuma.

Amesema tayari Kampuni ya TANZANICE imeahidi kununua tangawizi toka kwa wakulima wa Madaba ,na kwamba matarajio ya Halmashauri siku zijazo ni kupata msindikaji mkubwa.

Hata hivyo amesema Halmashauri imejipanga kuwahamasisha wakulima  wanaoweza kulima na kusindika zao hilo ambapo amejitokeza Mkulima mmoja toka Kijiji cha Ifinga kulima na kusindika zao hilo.

Amesema ni azma ya Halmashauri hiyo kwa kushirikiana na  wadau mbalimbali kununua na kusindika tangawizi  ili zao hilo liendelee kuongeza uchumi wa Madaba na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Afisa Habari Halmashauri ya Madaba

Desemba 7,2020

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa