• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

TANESCO Ruvuma yasambaza umeme vijiji 119

Posted on: July 8th, 2021

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO)  mkoani Ruvuma kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) limefanikiwa kusambaza umeme katika vijiji 119 kati ya lengo la kusambaza umeme vijiji 161.

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Florence Mwakasege amesema mradi huo umetekelezwa kupitia REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza ukihusisha pia ujenzi wa njia mbili za umeme wenye urefu wa Kilometa 106 kuelekea kituo cha kufua umeme wa maji Nakatuta Mto Ruvuma.

Amezitaja gharama za mradi huo kuwa ni zaidi ya shilingi bilioni 43 na kwamba vijiji ambavyo bado havijasambaziwa umeme utekelezaji wake upo katika hatua mbalimbali.Mhandisi Mwakasege amesema tayari wateja 5,902 wa awali wameunganishiwa kati ya lengo la kuunganishiwa wateja 6,178 mradi huo utakapokamilika kwa asilimia 100

Amesema Mkoa wa Ruvuma una jumla ya vijiji 551,kati ya hivyo vijiji vyenye umeme ni 295,vijiji visivyo na umeme vilivyoomba kupitia  REA awamu ya tatu mzunguko wa pili 256 na vijiji vitakavyokuwa na umeme baada ya miradi inayoendelea kukamilika ni 295.

Hata hivyo amesisitiza kuwa hadi kufikia Desemba 2022 vijiji vyote ambavyo havijapatiwa umeme katika Mkoa wa Ruvuma vinatarajiwa kumfikiwa na umeme.

Kuhusu upatikanaji wa umeme mkoani Ruvuma,Mhandisi Mwakasege amesema upatikanaji wa umeme ni wa kuridhisha baada ya Mkoa kuunganishwa na Grid ya Taifa katika Wilaya za Songea,Namtumbo,Mbinga,Nyasa na Tunduru.

“Mkoa wa Ruvuma pia unapata umeme kutoka kwa wawekezaji binafsi wa Kampuni  za Tulila na Andoya ambao wana uwezo wa kufua umeme megawati 5.5 na kuingiza kwenye Grid ya Taifa’’,alisema Mwakasege.

Amewataja wateja waliounganishiwa umeme katika kipindi cha Julai 2020 hadi Machi 2021 kuwa ni 7,411 ukilinganisha na lengo la mwaka la kuunganisha wateja 6,000 sawa na asilimia 123.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Julai 6,2021

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa