TAASISI ya kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma wamejipanga kufanya uchunguzi Katika Halmashauri zote katika Upotevu wa fedha zaidi ya bilioni 3 katika mfumo wa mashine za Pos.
Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Hamza Mwenda amesema wameendelea kutekeleza majukumu yake katika robo ya nne ya mwaka wa fedha 2020/2021 iliyoanzia Aprili hadi Juni 2021.
“Vipaumbele vya kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba kufanya uchunguzi wa hoja ya Mdhibiti na mkaguzi wa Hesabu za Serikali katika ubadhilifu wa fedha katika Halmashauri kupitia utaratibu wa POS”
Mwenda amesema katika kipindi hicho cha mienzi mitatu wamefuatilia matumizi ya fedha za umma katika utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo (PETS)na kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa viwango kinachotakiwa na thamani ya fedha inapatikana kwa kuzuia mianya ya rushwa na upotevu wa rasilimali katika Utekelezaji.
Hata hivyo amesema katika hatua nyingine TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma imefanikiwa kufanya ufuatiliaji wa Miradi 5 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi bilioni 1 na mapungufu yaliyobainika yametolewa mapendekezo na maboresho kwa mamlaka husika na yameanza kufanyiwa kazi.
TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma katika kipindi cha miezi mitatu wamepokea taarifa 110 kutoka kwa wananchi kupitia vyanzo mbalimbali na malalamiko yote yalifanyiwa kazi taarifa 39 zilikuwa za rushwa na taarifa 71 hazikuhusu rushwa hivyo watoa taarifa walishauliwa namna bora ya kutatua kero zao.
“TAKUKURU inayotembea tumeweza kusikiliza kero za wananchi katika maeneo mbalimbali na kutatua kero hizo katika kijiji cha Ndongosi Halmashauri ya Wilaya ya Songea na Maweso Halmashauri ya Mdaba”.
Mwenda amesema wamepokea malalamiko 8 yalihusu ubadhilifu katika vyama vya msingi vya ushirika –AMCOS,Migogoroya ardhi,ubadhilifu wa fedha kupitia force account,matatizo ya mirathi na viongozi wa vijiji kutooa taarifa za mapato na matumizi ya fedha za vijiji.
Mwenda amesema wamejipanga kuongeza uelimishaji Umma kwa kutumia njia mbalimbali kushiriki katika maonesho ,mbio za mwenge matamasha ya uelimishaji,semina kwa watendaji pamoja na kufanya chambuzi za mifumo katika maeneo yanayolalamikiwa zaidi kama maeneo ya utoaji wa huduma katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo sekta ya Elimu,Ununuzi,Kilimo na Afya.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Mdaba
30,Julai 2021
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa