TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma katika kipindi cha Robo mwaka kuanzia januari mpaka Machi imejipanga kuelimisha jamii, kupiga vita rushwa kwa kutokuwa sehemu ya wanaoshiriki rushwa.
Akitoa taarifa ya robo mwaka ya Oktoba hadi Desemba 2020 kwa waandishi wa Habari katika kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa ofisi ya Takukuru Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ruvuma Hamza Mwenda amesema wataendelea kufuatilia miradi ya Serikali inayoendelea kutekelezwa katika hatua mbalimbali ili kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana katika miradi hiyo.
“kipindi cha kuanzia mwezi oktoba mpaka Desema 2020 ofisi ya Takukuru Mkoa wa Ruvuma jumla ya taarifa 170 kutoka kwa wananchi kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo kesi zilizoendelea Mahakamani na kesi zilizofunguliwa’’.
Mwenda amesema katika kipindi cha mwezi Oktoba hadi Desemba 2020 Takukuru Mkoa wa Ruvuma imefanikiwa kuokoa fedha zaidi ya shilingi milioni 50 kutokana na uchunguzi mbalimbali zilizofanyika.
Hata hivyo amesema Takukuru Mkoa wa Ruvuma imefanikiwa kufuatilia miradi ya maendeleo 10 ili kujilidhisha iwapo fedha hizo zilizotengwa kwaajili ya utekelezaji wa miradi husika zinatumika kadri ilivyokusudiwa.
Amesema miradi hiyo iko katika sekta za ujenzi wa miundombinu ya maji,Barabara,Elimu na huduma za Vikundi,yenye thani ya jumla ya shilingi Bilioni Moja.
Katika kuendelea kutekeleza jukumu la kushirikisha na kuelimisha Jamii kupambana dhidi ya Rushwa,Takukuru Mkoa wa Ruvuma katika kipindi hicho imefanya semina 52,Mikutano ya Hadhara 68,kazi 164 na kuimalisha klabu za wapinga rushwa kwenye shule za Msingi na Sekondari Mkoani Ruvuma.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Madaba
Januri 26,2021
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa