KAMATI ya Kudumu ya Bunge utawala Katiba na Sheria inayoongoza Wizara tano wametembelea ujenzi wa soko linalojengwa kwa shilingi Milioni 190 kupitia mradi wa TASAF Jimbo la Madaba Mkoa wa Ruvuma.
Akizungumza Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala bora Ridhiwani Kikwete amesema anatambua mchango mkubwa wa Rais Samia kwa kuwaletea ujenzi wa soko ikiwa mwanzo wananchi walikuwa wanapata shida eneo la kufanyia biashara.
Hata hivyo Kikwete amesema makubaliano katika ujenzi wa soko hilo ni hatua ya kwanza ikiwa masoko ya kisasa yanakuwa na maduka hivyo Serikali itahakikisha inaendelea kuleta fedha kwaajili ya ujenzi wa vizimba vya samaki na maduka.
“ Soko hili la Madaba tunataka liwe la mfano ili wananchi waje kujifunza madaba”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Machi 14,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa