• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

SIPO tayari kuona Mkoa unakuwa nyuma Kielimu RC Ruvuma

Posted on: January 22nd, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewaagiza wakuu wa shule za  msingi na sekondari kuhakikisha wanainua  kiwango cha ufaulu kwa  wanafunzi  na kuunasua Mkoa kwenye ufauli usioridhisha ambao umedumu kwa kipindi cha miaka mitatu.

Kanali Thomas ametoa agizo hilo  wakati anazungumza kwenye kikao kazi  na walimu wakuu  wa shule za msingi na wakuu wa shule za sekondari  kilichofanyika kwa nyakati tofauti kwenye ukumbi wa sekondari ya Songea.

“Mtambue kuwa sisi viongozi wenu hatupo tayari kuuona Mkoa unaendelea kufanya vibaya katika sekta ya elimu,hivyo tumieni kikao hiki kuwa chachu ya kufanya mabadiliko,mwaka huu tuanze kwa kufanya mabadiliko makubwa katika utendaji wetu wa kazi ’’,alisisitiza RC Thomas.

Ametahadharisha baada ya kikao hicho hatasikiliza kisingizio chochote kwa matokeo yasiyoridhisha kwenye mitihani ya kitaifa ambapo amewaagiza wakuu hao kujirekebisha na kufanya tathmini ya utendaji kazi ili kuongeza uwajibikaji.

Ili kuhakikisha ufaulu katika elimu ya msingi na sekondari unaongezeka Mkuu wa Mkoa amewaagiza wakuu wa shule kusimamia na kuinua taaluma katika shule zao.

Mkuu wa Mkoa pia ameagiza miradi ya ujenzi kusimamiwa ipasavyo na kusimamia fedha za serikali zinazotolewa kwa uendeshaji wa shule.

Maagizo mengine ambayo ameyatoa ni kila shule kupanda miti ya matunda,kushirikiana na jamii katika kuleta maendeleo ya shule,kuboresha mazingira ya shule,kujiepusha na mikopo inayotolewa na Taasisi zisizo za kibenki na kutekeleza agizo la kila shule kulima hekari tano za mazao ya nafaka,mbogamboga na matunda.

Awali akitoa taarifa ya elimu ya msingi na sekondari kwenye kikao hicho,Afisa Elimu wa Mkoa wa Ruvuma Mwl,Edith Mpinzile amesema Mkoa umeendelea kufanya vibaya kwenye matokeo ya mtihani wa kitaifa kwa kuwa Mkoa umeshindwa kufikia lengo la ufaulu lililowekwa kitaifa la asilimia 85 kwa mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi na asilimia 100 ya upimaji wa mitihani ya darasa la nne.

Ameutaja ufaulu wa darasa la saba mwaka 2023 ulikuwa ni asilimia 69.9 na ufaulu wa darasa la nne ni asilimia 76.01 ambapo amesema Mkoa pia umeendelea kufanya vibaya katika mitihani ya sekondari  ya kitaifa kwa kuwa Mkoa umeshindwa kufikia lengo la ufaulu la asilimia 100 kwa mtihani wa upimaji wa kidato cha pili ambapo ufaulu wa Mkoa mwaka 2023 ulikuwa ni asilimia 81.96.

Hata hivyo amesema Idara ya Elimu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imebaini mambo mbalimbali yanayosababisha ufaulu usioridhisha ambayo ameyataja kuwa ni baadhi ya walimu wanashindwa kutekeleza majukumu yao ya kila siku,mada hazikamilishwi na walimu hawatoi mazoezi na majaribio ya kutosha.

Changamoto nyingine amezitaja kuwa ni baadhi ya walimu hawazungumzi na wanafunzi kujua changamoto zao,walimu hawakai kwenye vituo vya kazi,walimu hawana ubunifu na walimu kuwa na madeni yaliyopitiliza ambayo yanaondoa utulivu kazini hivyo walimu wanashindwa kufundisha kikamilifu.

Mkoa wa Ruvuma una shule za msingi  841 na shule za sekondari 233

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa