TATHIMINI ya hali ya Elimu Halmashauri ya Madaba katika shule za sekondari, ilivyoongoza miaka mitatu mfululizo licha ya kuwa na watumishi wachache.
Akitoa haarifa hiyo kaimu afisa Elimu Sekondari Devis Mwasi amesema idara ya Elimu Sekondari inajumla ya shule za Sekondali 11 kati ya hizo 8 za serikali na 3 za binafsi,2 ni shule za kidato ya tano na sita, wanafunzi 3391 kati ya wanafunzi 2727 ni wa shule za serikali na wanafunzi 666 ni washule za binafsi.
Mwasi amesema idara ya Elimu inajumla ya watumishi 137 na inauhitaji wa watumishi 182 kati ya hao walimu wa sanaa walimu 114 na walimu wa masomo ya sayansi 68.
Kaimu afisa Elimu akitoa ripoti ya wanafunzi wa kidato cha kwanza walioripoti na wasioripoti amesema Halmashauri ya Madaba ilipangiwa jumla ya wanafunzi 1148 kati ya shule 8 za kutwa kati ya hao wanafunzi walioripoti hadi kufikia machi 30 2021 ni 949 sawa na asilimia 82.7 na wasiripoti asilimia 17.3.
Amesema Mwongozo wa Wizara ya Elimu unaelekeza kuwa mwanafunzi akichaguliwa kuingia kidato cha 1 au 5 atakosa nafasi yake baada ya miezi 3,hapo bodi ya shule inatakiwa ikae na kufanya maamuzi kuwafuta shule wanafunzi hao.
“Miundo mbinu na samani ya shule za Sekondari mahitaji ni madarasa 86 yaliyopo 83,Nyumba za walimu 137 zilizopo 40 upungufu 97,maabara 24 zilizopo 9 upungufu 15,matundu ya vyoo 133 yaliyopo 73 upungufu 60,Meza 2725 zilizopo 2725 hakuna upungufu,pamoja na viti 2725 vilivyopo 2711 upungufu 14”.
Hata hivyo Afisa Elimu amesema hali ya Taaluma katika shule za Sekondari inaridhisha pamaoja na kuwepo kwa changamoto,matokeo ya utoaji taaluma ambayo yanapimwa kwa hali ya ufaulu wa mitihani ya kitaifa na ndani ya kidato cha pili ni mzuri na kitado cha nne ni wastani wa kidato cha sita.
Halmashauri ya Madaba shule 10 ambazo zilikuwa na watahiniwa wa kidato cha 2 2019 ilikuwa na jumla ya 714 na ufaulu ulikuwa mzuri asilimia 95.25 na ufaulu huo umepelekea halmashauri ya madaba kushika nafasi ya kwanza kati ya hamashauri 8 za Mkoa wa Ruvuma.
Mwasi akielezea changamoto za wanafunzi ni utoro,wanafunzi kukaa mbali na shule ikiwemo shule ya Nguluma na Gumbiro, ukosefu wa miundombinu inayokidhi mahitaji ya utoaji wa Elimu,upungufu wa walimu wa sayansi,sanaa na Hisabati,fizikia,kemia,biolojia na kilimo pamoja na kukosekana nyumba za kuishi walimu.
Changamoto ngazi ya Halmashauri kuwepo kwa ufinyu wa bajeti za kuratibu na kusimamia shughuli za elimu na fedha za maendeleo,kukosekana kwa usafiri kwaajili ya ufuatiliaji na upungufu wa vitendeakazi kama kompyuta,karatasi na wino.
Imeandaliwa na Aneth ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Madaba
April 13,2021.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa