Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wamefanya tathimini ya Mtihani wa utamilifu wa Wilaya wa Darasa la Saba.
Tathimini hiyo imefanyika katika Shule ya Msingi Madaba ikiwa shule ya Msingi St Getrude imeongoza kwa asilimia 100 ikifuatia Shule ya Msingi Mkwera asilimia 84.21.
Hata hivyo Mwalimu wa Shule ya St Getrude January Nyongole ameeleza sababu inayopelekea kuchukua nafasi ya kwanza kila mwaka ikiwemo mahusiano mazuri kazini Mwalimu Mkuu na walimu wengine, Mitihani ya mara kwa mara pamoja na kufanya tathimini kila wiki baada ya Mtiahni.
Afisa Elimu Taaluma Rashid Hashim Pili Halmashauri ya Madaba Kufuatia tathimini hiyo amesema Kata ya Mkongotema imeongoza kwa asilimia 72.58 na nafasi ya pili imechukua Kata ya Lituta kwa asilimia 62.56,pamoja na Kata ya Matumbi kuwa nafasi ya mwisho kwa asilimia 16.33.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ifinga Erasmo Mlowe mara baada ya kupokea matokea amekili kuyapokea na kuahidi kubadilika katika matokea ya mitihani ijayo.
Hata hivyo ameeleza changamoto ikiwa ni pamoja na upungufu wa walimu katika shule nzima kuwa na walimu 3 na kusababisha mzigo mzito wa Vipindi katika ufundishaji kwa Walimu hao.
Afisa Elimu Halmashauri ya Madaba Saada Chwaya kufuatia changamoto alizotoa Mwalimu wa Shule ya Msingi Ifinga amesema amekwisha peleka walimu 2 na wamesha lipoti katika Shule hiyo.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Mei 4,2023
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa