HALMASHAURU ya Madaba imepokea kiasi cha fedha shilingi milioni 470 kwaajili ya ujenzi wa Shule ya Joseph Kizito Mhagama Desemba 21,2022.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed ametoa taarifa hiyo amesema fedha hizo kwaajili ya ujenzi wa jengo la Utalawa,vyoo 20, Maabara 3, Maktaba 1 Chumba cha Tehama kimoja na madarasa 8.
Amesema fedha zilizoingizwa katika akaunti ya Shule ya Sekondari ya Madaba kupitia program ya SEQUIP ya ujenzi wa Shule 1000 za Sekondari Tanzania nzima.
Hata hivyo Mkurugenzi amesema kutokana na miongozo ya utekelezaji wa mradi huo ulitambulishwa Januari 24,2022 na kuanza kutekelezwa Machi 14,2022 kwa kufuata miongozo iliyotolewa.
“Hadi kufikia Novemba 25 ,2022 fedha zilizotumika ni kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 468 na kubakiwa na shilingi zaidi ya milioni moja na kufikia hatua ya ukamilishaji”.
Amesema mradi umefikia asilimia 95 kwa ujenzi wa madarasa 8 jengo la utawala 1 vymba 3 vya maabara ,matundu 20 ya vyoo,minara 2 ya tenki,mfumo mmoja wa kunawa mikono na asilimia 65 kwa jengo 1 la maktaba na chumba 1 cha ICT na mradi unatarajiwa kukamilika kwa asilimia 100 ifikapo Desemba 30,2022.
Mkurugenzi ameeleza namna ambavyo wananchi wa Kata ya Lituta walivyoshiriki kuchangia nguvu zao katika uchimba wa mitaro ya maji na ujazaji wa kifusi ambapo ni sawa na thamni ya shilingi laki 8.
Ameelezea changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa mradi huo ubovu wa barabara ambao ulisababisha gharama ya usafirishaji wa vifaa kuwa kubwa kwa kutumia trekta.
Ukosefu wa umeme ikiwa pamoja na kutumia jenerata pamoja na maji ya kutosha na vifaa vya ujenzi kama vile bati na kokoto.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa