• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

SERIKALI yatumia bilioni 7.7 kujenga Sekondari za mfano 11 ruvuma

Posted on: November 27th, 2022

SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imejenga shule mpya 11 za sekondari mkoani Ruvuma zilizogharimu shilingi bilioni 7.7.

Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Mipango  katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Jumanne Mwankoo amezitaja shule hizo mpya kuwa  zimejengwa katika Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma.

Amesema shule hizo zimejengwa kupitia mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari nchini (SEQUIP) ambapo kila Halmashauri imejengwa shule moja kwa thamani ya shilingi milioni 470.

Hata hivyo amesema katika Halmashauri ya Tunduru zimejengwa shule tatu za sekondari kupitia mradi wa SEQUIP na kwamba katika Halmashari ya Namtumbo pia zimejengwa shule mbili ikiwemo shule ya wasichana ya Mkoa iliyojengwa katika eneo la Migelegele kwa gharama ya shilingi bilioni  tatu.

“Mradi wa SEQUIP umewezesha kila shule ya sekondari kuwa na jengo la utawala,vyumba vya madarasa, vyoo,mfumo wa maji, maabara,maktaba na jengo la TEHAMA ,shule zote zinatarajia kuanza kuchukua wanafunzi Januari 2023’’,alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amekagua moja ya shule hizo katika Halmashauri ya Madaba.

Akitoa taarifa ya mradi wa shule hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed amesema mradi wa ujenzi  umetengewa shilingi milioni 470 na ulianza utekelezaji Machi 2022 ambapo hadi sasa fedha zilizotumika ni zaidi ya shilingi milioni 468.

Amesema ujenzi wa mradi huo upo katika hatua za ukamilishaji ambapo hadi sasa umefikia asilimia 95 ukihusisha ujenzi wa madarasa nane,jengo moja la utawala,vyumba vitatu vya maabara,matundu 20 ya vyoo,minara miwili ya matanki na mfumo wa kunawa mikono.

Hata hivyo amesema ujenzi upo katika asilimia 65 kwa majengo mawili ambayo ni jengo la  maktaba na chumba cha TEHAMA na kwamba mradi unatarajia kukamilika kwa asilimia 100 kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amemwagiza Mkandarasi kushughulikia dosari zote zilizojitokeza ikiwemo mipasuko kwenye kuta.

Amesema Rais ametoa fedha nyingi kutekeleza mradi huo hivyo ni lazima majengo yalingane na thamani ya fedha kwa kutekeleza mradi katika ubora na viwango.

Katibu Tawala wilaya ya Songea Pendo Ndumbaro ameahidi maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa kuyafanyia kazi ambapo amemwagiza Mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili kukamlisha mradi huo.

Serikali inatekeleza mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwa kujenga shule mpya za sekondari 1000 katika nchi nzima.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma

Novemba 27,2022

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa