KAMATI ya Fedha Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Lilondo inayojengwa kwa zaidi ya shilingi Milioni 560 kupitia mradi wa SEQUIP.
Msimamizi wa Mradi huo Mwalimu Godfrey Stephano akisoma taarifa kwa kamati hiyo amesema walipokea fedha Juni 6,2023 kwaajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Lilondo.
“Mradi huo unajengwa jengo la utawala,maabara 3,madarasa 8,maktaba 1,chumba cha Tehama,vyoo vya wasichana na wavulana,kichomea taka na tanki la maji la ardhini”.
Amesema ujenzi huo umefikia katika hatua mbalimbali ikiwemo kupiga lipu pamoja na wananchi wameshiriki katika hatua mbalimbali kusafisha eneo,kuchimba msingi,kujaza kifusi,uchimbaji wa mashimo ya vyoo.
“Mpaka kufikia sasa fedha iliyotumika ni zaidi ya shilingi milioni 300 na kiasi cha fedha kilichobaki ni zaidi ya shilingi Milioni 250”.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Novemba 7,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa