Serikali imetoa zaidi ya shilingi Bilioni moja kutekeleza miradi ya Boost na Swash Halmashauri ya Madaba.
Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji Sajidu Idrisa Mohamed amesema Halmashauri hiyo imepokea zaidi ya shilingi Milioni 610 kupitia mradi wa Boost kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule sita za Msingi.
Mohamed amebainisha zaidi kuwa Halmashauri hiyo imepokea zaidi ya shilingi Milioni 436 kupitia mradi wa SWASH kwaajili ya ujenzi matundu ya vyoo na uwekaji wa miundombinu ya maji katika shule za Msingi 11.
Hata hivyo miundombinu mingine inayotekelezwa kupitia mradi wa SWASH ujenzi wa kichomea taka,ujenzi wa placenta na ujenzi wa sehemu ya kunawia mikono katika Zahanati ya Ngumbiro.
“Kwa niaba ya wananchi wa Halmashauri ya Madaba tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hasan kwa kuendelea kutuletea fedha za kutekeleza miradi mbalimbaliya maendeleo”.
Amesema Shule ya Msingi Mahanje imefikia hatua ya Ukamilisha na kufikia asilimia 90 ya Mradi huo.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Julai 12,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa