SERIKALI imetoa shilingi Milioni 50 kwaajili ya ukamilishaji wa Zahanati katika kijiji cha Mahanje Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Kamati ya Fedha wametembelea na kukagua mradi huo wa zahanati uliofikia asilimia 80 na kutarajiwa kuanza kutoa huduma hivi karibuni.
Mtendaji wa kijiji cha Mahanje Jabiri Fusi akisoma taarifa kwa kamati ya Fedha amesema kazi zilizobakia ni pamoja na kufunga allumium madirisha yote,Kufunga milango,pamoja na kuweka malumalu baaddhi ya vyumba ikiwemo chumba cha kujifungulia wanawake.
“Mradi ukikamilika utasaidia kusogeza huduma kwa ukaribu kwa wananchi”
Hata hivyo Diwani wa Kata hiyo Stephano Mahundi amemshukuru Rais samia kwa kuwapatia fedha kwaajili ya ukamilishaji wa Zahanati hiyo pamoja na Mbunge wa Jimbo la Madaba kwa jitihada za kuhakikisha Kata hiyo inapelekewa miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Mei 17,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa