WATAALAMU kutoka ofis ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wametembelea na kukagua Miradi katika Halmashauri ya Madaba.
Moja kati ya Mradi huo waliotembelea ni Nyumba ya Mwalimu Shule ya Msingi Mtazamo Kata ya Mkongotema Kijiji cha Lutukila inajengwa kwa milioni 50.
Akisoma taarifa hiyo Makamu mkuu wa Shule hiyo Slavian Kingilo amesema mradihuo unatekelezwa kupitia fedha kutoka Serikali kuu na mradi huo umeanza kutekelezwa rasmi Novemba 29,2022.
Kingilo amesema mradi huo unatekelezwa kupitia utaratibu wa force account ambapo shule inanunua vifaa na kuajiri fundi ujenzi kwa mkataba wa muda mfupi wa ujenzi.
Hata hivyo amesema hatua ya ujenzi wa mradi huo umefikia katika hatua ya kupandisha kuta za juu ya lenta ikiwa jumla ya fedha zilizotumika mpaka kufikia sasa ni zaidi ya shilingi milioni 25.
“Faida za mradi huo nipamoja na kupunguza adha ya makazi kwa walimu,kuongeza tija na ufanisi wa kuinua taaluma mashuleni”.
Makamu Mkuu wa Shule hiyo amezitaja changamoto mbalimbali zilizojitokeza ikiwemo ukosefu wa maji katika eneo la ujenzi ambapo imeongeza gharama za ujenzi kwa kununua maji kwa gharama kubwa pipa moja shilingi 5,000/=, kupanda kwa ghara za vifaa vya ujenzi kama vile nondo,bati na Saruji.
Kingilo amesema utatuzi wa changamoto hizo ni pamoja na kutafuta wazabuni wenye gharama nafuu za vifaa ili kupunguza ongezeko kubwa la fedha iliyo nje ya BOQ.
Hata hivyo Makamu Mkuu wa Shule ametoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha kwaajili ya ujenzi wa nyumba ya Mwalimu ambayo ikikamilika itasaidia kutatua adha ya makazi kwa walimu.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Feburuari 17,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa