• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

SERIKALI yatoa bilioni saba kutekeleza miradi ya maji Ruvuma

Posted on: March 13th, 2021

SERIKALI ya Awamu ya Tano imetoa zaidi ya shilingi bilioni saba kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Maji Mkoani Ruvuma.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake mjini Songea,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme  amesema fedha hizo ni kwaajili ya miradi ya Wilaya za Songea,Mbinga na Tunduru.

“ Tunapokwenda kuadhimisha wiki ya Maji kuanzia Machi 16 hadi 22 sekta ya maji imefanya kazi kubwa sana ya kutekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya kumtua mama  ndoo maji kichwani’’,alsema Mndeme.

Amesema kupitia Wakala wa Maji Vijijini RUWASA  NA Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira SOUWASA,kazi kubwa imefanyika ambapo serikali  imetoa zaidi ya shilingi bilioni 7 kwaajili ya uwekezaji wa maji ndani ya Mkoa wa Ruvuma.

 Hata hivyo amesema hadi sasa fedha iliyopokelewa ni zaidi ya shilingi bilioni tano na kwamba kiwango cha usambazaji wa maji safi wilaya ya Songea kimeweza  kuongezeka kutoka asilimia 74 hadi asilimia 86.2.

Kwa mujibu wa Mndeme wilaya ya Mbinga imepokea zaidi ya shilingi bilioni moja na kwamba huduma ya maji imeongezeka kutoka asilimia 52.2 hadi asilimia 70.8 na wilaya ya Tunduru imepokea fedha zaidi ya shilingi milioni 600 na kiwango cha usambazaji maji kimeongezeka kutoka asilimia 55 hadi 66.

Hata hivyo Mndeme amesema licha ya mafanikio hayo kuna changamoto za vyanzo vya maji katika Manispaa ya Songea ambazo zinasababisha upungufu wa maji kutoakana na ongezeko kubwa la idadi ya watu  na mahitaji ya Maji yanaongezeka.

Amesema katika kukabiliana na changamoto hizo,Mkoa kupitia SOUWASA umefanya juhudi mbalimbali za kukabiliana na changamoto hizo ikiwemo kuhakikisha mtandao wa mabomba unawafikia  watumiaji maji kikamilifu.

Mndeme amewapongeza RUWASA Mkoa wa Ruvuma  kwa kupambana na kuhakikisha Maji yanapatikana Mijini na Vijijini katika Mkoa wa Ruvuma unakadiriwa kuwa wakazi    zaidi ya milioni  1.34.

Kwa upande wake Meneja wa RUWASA Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Rebman Ganshonga amesema katika kipindi cha kuanzia Julai mwaka  2019 hadi Februari 2021  RUWASA  Ruvuma imepokea zaidi ya shilingi bilioni 20 kutoka serikali kuu katika kutekeleza uboreshaji miradi ya maji.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Afisa Habari Halmashauri ya Madaba

Machi 13,2021.

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa