• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

SERIKALI yatoa bilioni 12.7 Ruvuma kutekeleza miradi ya Afya,Elimu na Uchumi

Posted on: October 20th, 2021

MKOA wa Ruvuma umepokea shilingi bilioni 12.7 sawa na asilimia 2.4 ya shilingi bilioni 635.68 ambazo zimeidhinishwa na TAMISEMI kwa ajili ya uboreshaji wa sekta ya Afya,Elimu na Uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge katika kikao kazi cha maandalizi ya utekelezaji wa mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19 ,kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea 

“Matumizi ya fedha hizi yameelekezwa kwenye maeneo ya vipaumbele yanayogusa wananchi moja kwa moja ili kuwaondolea kero katika na kupata huduma za afya,elimu na uwezeshaji wananchi kiuchumi na kuwakinga dhidi ya UVIKO 19”’alisisitza RC Ibuge 

Akifafanua kuhusu fedha hizo Brigedia Jenerali Ibuge amesema sekta ya elimu imetengewa shilingi bilioni 10.32 kati ya fedha hizo elimu msingi imetengewa bilioni 1.36 kwa ajili ujenzi wa vyumba 52 vya madarasa na elimu sekondari imetengewa bilioni 8.96 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 448 vya  madarasa kwa ajili ya kujiandaa kupokea wanafunzi wa wa kidato cha kwanza Januari 2022.

Kwa upande wa sekta ya afya Brigedia Jenerali Ibuge amesema jumla ya shilingi bilioni 2.38 zimetengwa kwa ajili ya kuanzisha mfuko wa huduma za dharura ,kujenga jengo la wagonjwa mahututi na kununua mitambo miwili ya huduma za mionzi.

Mkuu wa Mkoa ameziagiza Halmashauri zote kusimamia ujenzi wa madarasa ya sekondari na kwamba ifikapo Desemba 30,2021 pasiwepo na upungufu tena wa vyumba vya madarasa na kusisitiza kuwa Halmashauri ambayo itakuwa na upungufu itumie vyanzo vya mapato ya ndani kujenga madarasa Hayo .

RC Ibuge amewaagiza watendaji kwenye Halmashauri zote kuhakikisha kuwa wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo kuwashirikisha wananchi tangu hatua za awali za utambulisho wa miradi.

katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amempongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kupambana na UVIKO 19,zilizowezesha nchi kupata mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi trilioni 1.3 kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa IMF kwa ajili ya kampeni Maendeleo ya uchumi na mapambano ya UVIKO 19.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma 

Oktoba 20,2021

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa