SERIKALI imebadili matumizi eneo lililotengwa kwaajili ya ufugaji lenye hekta 4600 kijiji cha Ngadinda kuwa eneo la kilimo cha Mahindi ya njano.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile ametoa taarifa hiyo alipoongea na wananchi katika kijiji hicho eneo hilo ambalo serikali ilitenga kwaajili ya wafugaji kuacha na kuondoka mara moja katika eneo hilo.
Ndile amesema Madaba na Mkoa wa Ruvuma ni eneo la Kilimo na linategemewa kwa kulisha Taifa la Tanzania hivyo ameagiza kukamatwa kwa Ng’ombe watakao onekana katika Wilaya ya Songea na kutozwa faini.
“Hakuna Ng’ombe yoyote kuingia Madaba wananchi naomba mtupe ushirikiano kwa kutoa taarifa mara moja mkiona Makundi ya Mifugo katika Maeneo yenu”.
Mkuu wa Wilaya ameipongeza Serikali kwa uamuzi wa kubadili matumizi ya eneo la Ufugaji kuwa eneo la Kilimo ambalo litasaidia upatikanaji wa mahindi ya njano kwaajili ya kulishia mifugo Tanzania na kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Juni 6,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa