UONGOZI wa Shule ya Sekondari Wino Halmashauri ya Madaba wameipongeza Serikali kwa kuwapelekea fedha zaidi ya shilingi Milioni 402 kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya Shule Mwaka wa fedha 2020/2023.
Akisoma taarifa Mkuu wa Shule hiyo Kelvin Mwinuka katika sherehe za Mahafari ya 15 ya kidato cha nne yaliyofanyika leo Shuleni hapo wanafunzi 113 wanatarajia kuhitimu mwezi Novemba 2023.
Mwinuka amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama kwa kuwanunulia wanafunzi Runinga ya Shule ambayo inawasaidia kuangalia habari mbalimbali zinazoendelea katika nchi ya Tanzania.
“Wino Sekondari tumepokea kiasi cha shilingi 402,072,379.85 kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya Madarasa,bweni la wavulana,nyumba za Walimu na Miundombinu ya Maji pamoja na ukamilishaji wa bwalo la chakula”.
Hata hivyo Mkuu wa Shule hiyo ameendelea kuwapongeza wadau mbalimbali akiwemo Wakala wa Misitu Wino (TFS) kwa kutatua changamoto mbalimbali kama vile ujenzi wa chanzo cha Maji,viti na Meza kwaajili ya Walimu,upandaji miti na utunzaji wa Mazingira.
Kwaupande wake Meneja wa Shamba la Miti Wino Grory Fotnatus akiwakilishwa na Afisa Misitu Geofrey Shio amesema kupitia changamoto zilizopo shuleni hapo watakarabati jengo la utawala wakisaidiana na wazazi kupitia zoezi la keki ambapo zimepatikana kiasi cha zaidi ya shilingi laki nane katika mahafari hayo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Madaba Teofanes Mlelwa amemwakilisha Mgeni rasmi katika Mahafari hayo Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama akiwa Amerca Kusini akiliwakilisha Bunge la Tanzania na Spika wa Bunge Tulia Akson.
Mlelwa amewapongeza wanafunzi hao kwa kutimiza miaka mine wakiwa shuleni hapo na kuwasisitiza kusoma mda uliobaki ili waweze kufaulu masomo yao ikiwa mwaka 2022 Matokeo ya kidato cha nne katika shule hiyo walipata asilimia 100.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Octoba 5,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa