WATAALU kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wametembelea mradi wa Darasa moja katika Shule ya Sekondari Magingo.
Mkuu wa Shule hiyo Said Kunemka amesoma taarifa ya mradi huo wa darasa moja uliokamilika kwa asimilia 100 umetekelezwa kwa shilingi milioni 20 fedha kutoka Serikali kuu.
Mkuu wa Shule hiyo amesema mradi huo uliaza kutekelezwa rasmi Octoba 24,2022 na kukamilika Desemba 4,2022.
“Mpaka sasa ujenzi umekamilika kwa asilimia 100 na umeghalimu kiasi cha shilingi milioni 20 hakuna salio lililobaki”.
Kunemka amezitaja faida za mradi huo ikiwa ni pamoja na kupunguza tatizo la madarasa,meza na vita,kuwezesha uandikishaji wa wanafunzi wa kidato cha kwanza waliopangwa kujiunga 2023 katika Shule hiyo.
Kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani,kuamsha ari ya wanafunzi kujifunza pindi wawapo Shuleni,upatikana wa samani bora kwa wanafunzi wakati wa kujifunza.
Kunemka ameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ambavyo vinaendelea kuleta tija ya kuboresha mazingira ya kujifunzia mashuleni.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba.
Feburuari 17,2023
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa